Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Bi. Erica Yegella amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkurugenzi mpya Ndg. Reuben Sixbert Jichabu Octoba 2, 2023.
Hafla ya makabidhiano imefanyika katika Ukumbi wa Jengo la Utawala Halmashauri ya Mji Masasi, ikishuhudiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji, Mhe. Hashim Namtumba, Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mhe. Geoffrey Mwambe, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara, Wazee wa mila, Wakuu wa Idara na Vitengo.
Katika hafla hiyo, Mkurugenzi mpya wa Halmashauri Ndg. Jichabu amemshukuru Mhe, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Mji Masasi huku akiahidi kutoa ushirikiano wa dhati wa watumishi, viongozi na wananchi wote.
Aidha amesema halmashauri itakwenda kukusanya mapato kwa mujibu wa kanuni, taratibu, sheria na miongozo ili utekelezaji wa miradi ya maendeleo uweze kutimia na kukamilika kwa wakati.
"“Miradi yote tuliyokabidhiwa tutaifanya kwa kasi na muda uliokusudiwa, tunakwenda kukusanya mapato, ninaomba mnipe ushirikiano, napenda kutumia akili zaidi, halmashauri hii tunahitaji kukusanya mapato ili shughuli za maendeleo ziendelee, tupo tayari kutatua changamoto zote za wananchi”
Kwa upande wake Bi. Yegella amemshukuru Mhe. Rais kwa Kumuamini katika nafasi mbalimbali za uteuzi huku akibainisha kuwa halmashauri inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo fedha ipo kamilifu kama ujenzi wa shule ya Jida, shule ya sekondari Temeke ( nyumba ya walimu 2 in 1), hospitali ya Mkomaindo na shule ya Sekondari ya Wasichana ya Masasi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.