Julai 1, 2019 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bi.Gimbana Ntavyo wakiambata na Katibu Tawala Wilaya ya Masasi Ndg.Azizi Fakhi, Kaimu mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi Mhe.Mbaraka Kodo pamoja na Katibu wa CCM Wilaya ya Masasi Ndg. Shaibu Mtawa walikabidhi mkopo wa TZS.59,500,000 ikiwa ni sehemu ya asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kwa vikundi vya ujasiriamali vya Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu.
Awali Halmashauri ya Mji Masasi ilitoa mkopo wenye thamani ya TZS 20,000,000 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na hivyo kufanya jumla ya mkopo uliotolewa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kuwa TZS 79,500,000 ikiwa ni 10% ya mapato ya ndani.
Vikundi vilivyo nufaika na mkopo huo ni vikundi vya walemavu TZS.6,500,000/=, vikundi vya wanawake TZS.21,500,000/= pamoja na vikundi vya vijana ambao walikabidhiwa pikikpiki kumi na nne(14) zenye thamani ya TZS.31,500,000/=
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bi.Gimbana Ntavyo alieleza kuwa Halmashauri ya Mji Masasi haipo nyuma kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi kwa kuwa ndio chama tawala kilichoshinda uchaguzi wa mwaka 2015
Pia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi asisitiza mambo yafuatayo kwa vikundi hivyo,
Kwamba, “vijana wa kike wachangamkie fursa hii kwa kuwa wengi wao bado mwamko wao ni mdogo”pia alisema kuwa kila mwanakikundi awe na kitambulisho cha ujasiriamali.
Wakati wa kukabidhi hundi za mkopo huo wa thamani ya TZS.59,500,000/=, Katibu Tawala Wilaya ya Masasi Ndg.Azizi alisisitiza kuwa maafisa maendeleo ya jamii wajipange kuhamasisha vijana wa kike waunde vikundi na kupata mikopo na wanaopata mkopo ni lazima wawe na nidhamu ya pesa ili wamudu kufanya marejesho.
Kwa upande mwingine Katibu Tawala Ndg.Azizi Fakhi alipokuwa akikabidhi pikipiki kwa vikundi hivyo aliwashauri vijana wa bodaboda wafanye kazi kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na wasiendeshe wakiwa wamelewa.
Mwisho Katibu wa CCM Wilaya ya Masasi Ndg.Shaibu Mtawa alimpompongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bi.Gimbana Ntavyo kwa kazi kubwa inayoifanya katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapindi (CCM).
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.