• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe za Watumishi |
Masasi Town Council
Masasi Town Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisa Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Mji Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha
    • Machapisho
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Biashara
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Utawala na Utumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango miji na mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Makataba ya Picha

MILIONI 399 ZATOLEWA KWA VIKUNDI 75 MASASI MJI, AWAMU YA KWANZA MIKOPO YA ASILIMIA 10.

Posted on: January 26th, 2025

Jumla ya Tsh Milioni 399 zimetolewa kwa vikundi 75 katika Hafla ya Utoaji wa Mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu iliyotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani Halmashauri ya Mji Masasi kwa awamu ya kwanza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuridhia na kurejesha mikopo hiyo ili kuwasaidia wananchi kiuchumi.

 Akizungumza leo, Januari 26, 2025 katika hafla iliyofanyika  katika Ukumbi wa  Chuo cha Maendeleo FDC,  Mgeni rasmi, Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mhe. Geoffrey Mwambe amewataka kwenda kuitumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kufanya biashara kwa ufanisi ikiwemo kutunza hesabu vyema ili uwezeshaji kwa wananchi kiuchumi uliokusudiwa uwe na matokeo Chanya. 

“ Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha mikopo hii, lengo letu ni kuhakikisha uwezeshaji wa wananchi wa Masasi kiuchumi unafanikiwa. Kwa wananchi wetu, Tunazo fursa nyingi sana mbali na mikopo hii, ikiwemo TFS kuna mfuko wa uendelezaji wa misitu (TFF) wa kutoa ruzuku, uvunaji wa asali na shughuli mbalimbali za Halmashauri kama ujenzi n.k na nahimiza vikundi hivi kwenda kujisajili na Mfumo wa Manunuzi ya Umma (NeST) ili vipate kazi mbalimbali za Serikali” amesema. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu amewahimiza  wanufaika kuhakikisha wanarejesha fedha hizo kwa wakati ili ziweze kutolewa kwa vikundi vingine na tayari hadi sasa kupitia mapato ya ndani zaidi ya milioni 200 zimechangiwa kwenye mfuko wa maendeleo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa ajili ya awamu inayofuata. 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi Mhe. Hashim Namtumba amesema waheshimiwa madiwani wamefanya kazi muhimu kuhakikisha mikopo hiyo inatolewa ili kuwezesha ustawi wa wananchi na kwamba hakuna kikundi kilichopata kwa upendeleo na hivyo vikundi vyote vikawe mabalozi wa kusema mazuri ya Serikali na Halmashauri kwa kuwa awamu nyingine ya mkopo inafuata.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Masasi, Mariam Kasembe amewahimiza wanufaika kuhakikisha hawatumii fedha hizo kinyume na malengo yaliyokusudiwa wakati wa kuunda vikundi na kuomba mikopo hiyo na kuacha shughuli zisizokusudiwa  ikiwemo kutumia kwenye sherehe.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Mratibu wa Mikopo hiyo, Ndg. Ebenezer Uisso amesema jumla ya vikundi 75 vimepata mkopo wa Tsh. millioni 399 kwa mchanganuo wa vikundi vya vijana 24 vimepata Tsh 160, 325, 000, vikundi vya wanawake 47 vimepata  Tsh  222,675,000 na watu wenye ulemavu vikundi 4 vimepata Tsh. milioni 16.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 28, 2020
  • TANGAZO LA KAZI April 05, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • Kuona Vyote

Habari Mpya

  • “VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA MKOA WA MTWARA TUWEKE KIPAUMBELE CHA UTOAJI WA HUDUMA ZA TIBA OKOVU NA HUDUMA MSINGI KWA WAGONJWA MAHUTUTI” RAS MTWARA.

    May 15, 2025
  • “WANANCHI TUJITOKEZE MKOMAINDO HOSPITALI KUPATA VIPIMO NA MATIBABU YA SARATANI BURE, SERIKALI IMELIPIA GHARAMA (SAMIA SULUHU OUTREACH SERVICES)” DC KASSANDA

    April 23, 2025
  • HISTORIA YAANDIKWA MASASI MJI, ZAIDI YA MILIONI 545 ZATOLEWA MWAKA HUU WA FEDHA 204/2025 KWA VIKUNDI 105 MIKOPO YA ASILIMIA 10.

    April 07, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA MASASI MJI WATOA ELIMU KUHUSU TAHADHARI YA UGONJWA WA MPOX

    April 06, 2025
  • Kuona Vyote

Video

SHERIA ZA MITANDAO
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Sheria ndogo ya Ada na Ushuru kwa Mji wa Masasi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Mtwara
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais UTUMISHI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • SALARY SLIPS PORTAL

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MASASI TOWN COUNCIL

    Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI

    Simu Ya Mezani: +255 23 2510685

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: info@masasitc.go.tz

Mawasiliano

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma Zetu

Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.