Mwenge wa uhuru leo April 9, umepokelewa Halmashauri ya Mji Masasi unakimbizwa Umbali wa km 81. Tarafa moja (1), kata saba (7), vijiji vitano (5) na mitaa kumi na saba (17).
Akizungumza katika mapokezi ya mwenge huyo Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Masasi Elias Ntiruhungwa amesema kuwa Mwenge wa uhuru utapitia jumlaya miradi mitano (5).
Aidha amesema kuwa katika miradi hiyo itakayopitiwa na mwenge wa uhuru mitatu (3) inawekwa jiwe la msingi, miwili (2) inakaguliwa na kuonwa ikiwa na gharama ya Shilingi 827,875,000.
Amesema fedha hizo Mchango wa Wananchi - sh 7,840,000,Halmashauri - Tshs. 112,000,000 • Wahisani - Tshs. 8,785,000 na Fedha kutoka Serikali Kuu -Tshs. 699,250,000.
Mkesha wa mwenge wa uhuru leo utakuwa uwanja wa Boma Masasi huku ukiwa na kaulimbiu inayosema Tunza mazingira okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa taifa.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.