Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano –Masasi Mji
Mhe.Festo Ndugange (Mb), Naibu Waziri OR-TAMISEMI amepongeza hatua zinazochukuliwa na uongozi wa Halmashauria ya Mji Masasi wakiongozwa na Mkurugenzi wake Ndg. Elias Ntiruhungwa katika usimamizi wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa inayotekelezwa chini ya programu ya Maendeleo ya Jamii na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Mhe.Ndugange ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea ujenzi wa miradi hiyo leo tarehe 27/11/2021 katika vituo vitatu tofauti ambavyo ni Shue ya Sekondari ya Wasichana Masasi, shule ya Sekondari ya kutwa Anna Abdallah na kituo kipya cha afya kinachojengwa Kata ya Mtandi.
Aidha Mhe.Ndugage amesisitiza kasi zaidi iongezwe ili ifikapo tarehe 15/12/2021 vyumba vyote vya madarasa viwe vimekamilika.
Halmashauri ya Mji Masasi ilipokea jumla ya fedha TZS milioni 820 kutoka katika Mpango wa Maendeleo ya Jamii na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 ambapo milioni 700 ni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 35 vya madarasa kwa shule za Sekondari, milioni 80 ni kwa ajili ya ujenzi wa bweni Shule ya Msingi Masasi kwa watoto wenye mahitaji maalum na milioni 40 ni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa kituo Shikizi kijiji cha Mkajamila.
Aidha Halmashauri ya Mji Masasi ilipokea TZS milioni 250 inayotokana na tozo za miamala kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha kimkakati Kata ya Mtandi.
Ujenzi wa vyumba vya madarasa umefikia hatua mbalimbali ambapo jumla ya vyumba 26 vipo katika hatua ya upauji, vyumba 11 vipo katika hatua ya ukamilishaji, ujenzi wa bweni upo katika hatua ya msingi na kituo cha Afya upo katika hatua ya ujenzi wa kuta.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.