Diwani kata ya Mumbaka Mhe. Hamisi Nikwanya amechaguliwa rasmi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi.
Awali akitangaza matokeo ya uchaguzi katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa mwaka, uliofanyika Agosti 5, 2023, Katibu Tawala Wilaya ya Masasi Bi. Fatma Kubenea ambaye ni mwenyekiti wa uchaguzi huo, amemtangaza Mhe. Nikwanya baada ya kupata kura za ndio.
Mhe Nikwanya amechaguliwa kwa kupigiwa kura za ndio au Hapana kwakuwa alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo.
“Jumla ya kura zilizotakiwa kupigwa ni 19, kura zilizopigwa ni 16 kura za ndio ni 12 na kura 4 ziliharibika” Mwenyekiti wa uchaguzi Bi. Fatma Kubenea.
Akitoa neno la shukurani Mhe Nikwanya amewashukuru waheshimiwa madiwani kwa kumchagua katika nafasi hiyo na kuahidi kuwa ataimarisha ushirikiano baina ya madiwani na watendaji wa halmashauri ili malengo ya halmashauri ya mwaka 2023/2024 yaweze kutimia kwa ukamilifu.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti aliyepita, Mhe. Mbaraka Kodo ambaye ni diwani kata ya Nyasa amewashukuru waheshimiwa madiwani na watendaji wa halmashauri kwa kumpa ushirikiano bora katika kipindi chote cha uongozi wake.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.