Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi ,Mhe.Jumanne Sagini amehudhuria sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwa mwaka 2023 katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi kama mgeni Rasmi wa Ufunguzi wa maonesho hayo.
Ufunguzi huo umefanyika Agosti 1,2023 katika viwanja vya Nanenane Ngongo vilivyopo Mkoani Lindi.
Katika Maonesho hayo Mhe.Sagini ametembelea mabanda mbalimbali ya halmashauri eneo la Magereza,JKT na Tari Naliendele.mm
Akihutubia katika ufunguzi wake Mhe.Sagini amesema kuwa uwanja wa Ngongo ni uwanja wa Kimataifa ambacho ni cha Mfano wa kuigwa na maeneo Mengine pia ameusifu uwanja huo kuwa na miundombinu na Majengo bora.
“Uwanja wa Nanenane ni wa kimataifa na wakuigwa”Saginibb
Aidha ametoa pongezi kwa wakuu wa Mikoa yote miwili Lindi na Mtwara kwa kusimamia vizuri maandalizi ya Nanenane kanda ya kusini kwani maandalizi ni mazuri na yanavutia.
“Niwapongeze wakuu wa Mikoa yote miwili kwa kusimamia maandalizi haya kwa uweledi uwanja umesheheni Miundombinu bora ,Mabanda ya kutosha na yenye muonekano Mzuri”Sagini
Maonesho ya Nanenane kanda ya kusini yanajumuisha Mikoa miwili Lindi na Mtwara na yamefunguliwa Agost 1,2023 kilele chake Agost 8,2023.
Kauli Mbiu ya maonesho ya Nanenane 2023 kanda ya kusini inasema “Vijana na wanawake ni Msingi imara wa mifumo endelevu ya Chakula".
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.