Mratibu wa Mradi wa M-MAMA Bi. Lucia Libaba amesema mfumo wa M-Mama unahusisha usafirishaji wa mama wajawazito wanaojifungua ndani ya siku 42 na Watoto wachanga kuanzia siku 0 mpaka siku 28.
Amesema kundi hilo pindi wanapopata tatizo au dalili za hatari wanapaswa kufika eneo la kutibiwa kwa njia ya M-MAMA kwa kupiga simu Namba 115 ambapo utaulizwa maswali kadhaa kujua ulipo kisha wahusika wanawatafuta Madereva Jamii na kufika kubeba mgonjwa alipo.
Amesema hayo wakati wa zoezi la kugawa vitendea kazi kwa madereva jamii wapatao 15 kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji Masasi ambao wameingia mkataba na Mkurugenzi wa Mji Masasi kupitia Mfumo wa usafirishaji wa dharula kwa wakina mama wajawazito na watoto wachanga unaorahisisha mawasiliano na uchukuzi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mji Masasi, Kaimu Mganga Mkuu, Ndg. Benjamin Shilinde amesema wataendelea kuhakikisha madereva jamii wanapata stahiki za tripu kwa wakati pindi wanapokamilisha tripu ya kufikisha walengwa katika vituo kusudiwa.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.