Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg Abdallah Shaibu Kaim ameweka jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa barabara ya km 1-1 ya Tanesco -Yatima Halmasahauri ya Mji Msasi Mkoani Mtwara.
Mradi huo wa barabara ,ujenzi wa kalavati ,ujenzi wa mifereji kwa kutumia mawe na uwekaji wa alama za barabarani unaotekelezwa na Mkandarasi Makapo Contracts & General Co LTD chini ya Usimamizi wa ofisi ya Meneja wa Tarura wilaya ya Masasi.
Aidha gharama za utekelezaji wa Mkataba wa barabara ni Sh.Million 549.3 zikiwa ni pamoja fedha za maendeleo zinazotokana na tozo za Mafuta kwa bajeti yam waka wa fedha 2022/2023.
Mradi huo umekamilika kwa asilimia 98 ya utekelezaji ikiwa Mkandarasi yupo kwenye hatua za mwisho za ukamilishaji wa kazi zilizosalia.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.