Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Ndg Shaibu Abdallah Kaim apirl 9,2023 ameweka Jiwe la Msingi zahanati ya Kijiji cha Machombe Halmashauri ya Mji Masasi kata ya Marika.
Mradi huo ulianza kutekelezwa Septemba 4,2018 kwa nguvu za wananchi pamoja na Mfuko wa Jimbo ,huku mwaka 2022 Halmashauri ya Mji Masasi ilitoa fedha kwa ajili ya ukamilishji wa Mradi huo.
Mradi huo unakadiriwa kutumia kiasi cha Shilingi Milion 108.7 ,Mpaka sasa jumla ya fedha Shilingi Milioni 105.7 zimepokelewa wakati kiasi cha shilingi 95,165,678 zimetumika.
Aidha kwa mujibu wa taarifa za Mradi huu umelenga kuwasaidia wananchi wa Kijiji cha Machombe kata ya Marika kwa kupata huduma kwa wakati na kupunguza gharama za kutembea umbali mrefu wa Zaidi ya kilometa 10 kwenda kufata Matibabu katika Zahanatio za vijiji jirani vya Namatunu na Mumbaka.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa amemuomba Mkurugenzi wa Mji Masasi Ndg Elias Ntiruhungwa kukamilisha ujenzi huo kwa wakati kama ilivyopangwa ifikapo may 30,2023 ili wananchi waanze kufurahia huduma.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.