Wawakilishi kutoka Halmashauri ya Enzkreis ya nchini Ujerumani wamesema zawadi mbalimbali walizopewa kama ishara ya Upendo zinaakisi asili ya Masasi na hivyo kusaidia kutangaza utalii na fahari ya Masasi katika Halmashauri yao.
Akizungumza Julai 25,2023 kwa niaba ya Enzkreis ,Dkt.Hilde amesema kuwa inawapa nguvu kuendeleza ushirikiano baina ya halmashauri ya Mji Masasi na Halmashauri ya Enzkreis.
‘’Nina furaha sana kuwa nanyi hapa, zawadi hizi zinatupa tabasamu ,furaha,Nguvu ya kujiamini na Nguvu ya kuendeleza Ushirikiano wetu miaka inayokuja lakini pia niwatakie heri’’ Dkt .Hilde
Aidha Marafiki hao walikabidhi hati za umeme wa jua (solar) Nne kwenye Maeneo ambayo utekelezaji wa Miradi hiyo umekamilika ambayo ni Marika Sekondari ,Anna Abdallah Sekondari, Chuo cha Maendeleo ya Wananchi FDC na Zahati ya Nangose.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mji Masasi Bi. Erica Yegella amekabidhi zawadi kwa Marafiki wa Enzkreis kama Ishara ya upendo na kuimarisha uhusiano Mzuri na Zawadi ambazo zimetolewa ni pamoja na Maua ,Korosho,Vikombe na Vikapu.
‘’Tunakabidhi zawadi hizi kama ishara ya Upendo, Maua kama ishara ya Upendo wetu ,Korosho ni Biashara baina ya Halmashauri hizi mbili ,Vikapu kama ishara ya Asili na utamaduni wa Masasi, Vikombe vinatoa Ishara ya kuitangaza Halmashauri ya Mji Msasi na Picha zinataswira ya Mtoto wa kiafrika’’ Bi. Erica Yegella Mkurugenzi Mji Masasi.
Ushirikiano huo umeanza miaka 12 iliyopita ukijikita katika kuboresha Mazingira na Maisha ya wananchi wa Masasi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.