Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi, Bi. Erica Yegella amewahimiza wadau na wananchi kutembelea banda la Masasi Mji linalopatikana katika viwanja vya Nanenane Ngongo-Lindi ili kujionea teknolojia ya kisasa ya ufugaji, kilimo, uvuvi, fursa na bidhaa mbalimbali zinazopatikana katika banda hilo.
Amesema banda la Halmashauri ya Mji Masasi lina bidhaa bora zinazomuwezesha mtanzania kukua kifikra na kimaendeleo.
Amesema hayo Agosti 1, 2023 katika ufunguzi rasmi wa maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo- Lindi.
“Nawakaribisha wananchi wote mje katika banda la Halmashauri ya Mji Masasi, Kuna bidhaa zote kuanzia asali, jamii ya kunde, vikapu, mashine za kusaga na kukoboa, mashine za kupukucha mahindi, vifaa bora pamoja na elimu ya mifugo kutoka kwa madaktari bingwa wa mifugo” Bi. Erica Yegella.
Maonesho hayo yamefunguliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Jumanne Sagini agosti 1,2023 ambapo wadau mbalimbali wataonesha fursa za kilimo, mifugo na uvuvi hadi agosti 8, 2023.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.