Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Ndg. Reuben Sixbert Jichabu ameishukuru Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha programu ya kuwaletea wananchi Madaktari bingwa ambao hutoa huduma kwa wananchi moja kwa moja katika hospitali mbalimbali Nchini ikiwemo kambi maalumu ya Madaktari bingwa wa Mama Samia iliyofanyika Hospitali ya Mkomaindo.
Aidha amewakabidhi zawadi mbalimbali madaktari hao kama ishara ya shukurani kwa kazi waliyoifanya ya kusaidia wagonjwa mbalimbali kutoka Halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara.
Mganga Mfawidhi hospitali ya Mkomaindo, Dkt. Ditrick Mmole, amesema Hospitali ya Mkomaindo ilipokea jumla madaktari bingwa watano ambao ni Daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama, daktari bingwa wa magonjwa ya ndani, usingizi tiba na ganzi na daktari bingwa wa upasuaji.
Amesema zaidi ya wagonjwa 420 walipata huduma kambi ya madaktari Bingwa wa Mama Samia, ambapo daktari bingwa wa magonjwa wa akina mama aliona jumla ya wagonjwa 134, upasuaji 67, Watoto 94, wagonjwa wa ndani 125, upasuaji mkubwa mgonjwa mmoja.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.