Mwenyekiti wa Kamati ya Mpango wa kudhibiti ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Halmashauri ya Mji Masasi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mji Masasi Bi. Erica Yegella amesema ni muhimu kuangalia namna bora ya utoaji wa elimu dhidi ya ukatili wa wanawake na Watoto ili kumaliza changamoto ya ukatili katika jamii.
Ametoa wito huo Agosti 7,2023 katika kikao cha kamati ya MTAKUWWA robo ya nne 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa jengo la Utawala Halmashauri ya Mji.
Amesema Mpango wa Taifa wa kudhibiti ukatili dhidi ya wanawake na Watoto (MTAKUWWA) unatekelezwa katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Serikali za Mitaa kupitia watalaamu mbalimbali na wanajamii wote.
Amesema elimu ya ukatili katika jamii inatolewa lakini ni vyema sasa kutazama namna na mbiu za ufundishaji, uelekezaji na namna ya kufikisha na kupokea ujumbe wa ukatili ili jamii na wahanga wawe wazi kueleza changamoto wanazokumbana nazo.
“Mimi nafikiri tubadilishe namna ya ufundishaji na tukiwatumia viongozi wetu wa dini, vijana na hata kuunda klabu ya Mtakuwwa katika shule zetu za msingi, klabu inayoweza kujumuisha wanafunzi katika kila darasa, tutapiga hatua kubwa sana katika kupunguza ukatili” Mwenyekiti.
Amesema kasi ya utoaji elimu inapaswa kuongezeka ili jamii iwe na muamuko wa ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto
“lakini pia ni muhimu tupunguze ukatili na matukio yasiyopendezeka machomi kwa binadamu kwasababu wewe kama binadamu na elimu inakuwaje unaendeleza ukatili? mimi nataka tupunguze ukatili ili tufanye Masasi iwe sehemu ya kurelax, mtu akija hapa anaishi vizuri, anakula vizuri , analala vizuri, anatembea anasikia raha, Barabara safi kila kitu kinakuwa safi” Mwenyekiti.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Masasi, Dkt. Salum Gembe amesema katika kuhakikisha Mpango wa Taifa wa kudhibiti ukatili dhidi ya wanawake na Watoto (MTAKUWWA) unatekelezwa katika ngazi ya Halmashauri elimu ya ukatili wa kijinsia itazidi kutolewa kwa kushirikiana na dawati la jinsia kutoka Polisi, asasi za kiraia na jamii kwa ujumla.
Kikao cha MTAKUWWA robo ya Nne 2022/2023 kilihudhuliwa na wajumbe mbalimbali na wadau kutoka kwa wawakilishi wa makundi yote muhimu katika jamii ikijumuisha viongozi wa dini, wawakilishi kutoka makundi maalumu, mwakilishi wa Watoto na wanafunzi, watalaamu wa afya, kamati ya ulinzi na usalama, dawati la jinsia kutoka polisi, na maafisa elimu.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.