Kamati ya Fedha na Utawala Halmashauri ya Mji Masasi ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Hashim Namtumba imetembelea na kukagua vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuboresha na kuimarisha ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika vyanzo mbalimbali.
Kamati hiyo imetembelea na kukagua vyanzo hivyo, March 20-21, 2025 ambapo wametembelea standi mpya ya maegesho ya vyombo vya moto (magari) sambamba na vituo vya mafuta mbalimbali ambapo wamewasisitiza wamiliki wa vituo vya mafuta kuhakikisha magari hayalazwi katika vituo vyao kama ambavyo barua za zuio kutoka halmashauri walizopewa zinavyoeleza.
Aidha kamati hiyo imesisitiza ulipaji wa ushuru kwa wakati, upatikanaji wa dawa na huduma bora kwa wateja katika duka la dawa Mkomaindo, uimarishaji wa madini ya ujenzi, leseni za biashara sambamba na kusisitiza wale wanaokiuka taratibu na sheria na ulipaji wa ushuru kuchukuliwa hatua mbalimbali kwa mujibu wa sheria.
Kamati hiyo ilitembelea Vyanzo vya mapato vya maeneo mbalimbali ikiwemo uwanja Fisi, Sokosela, Tk magari madogo, wafanyabiashara wakubwa, vituo mbalimbali vya mafuta, mradi wa tofali, mradi wa standi ya Maegesho, madini ya ujenzi maeneo ya Matawale na Marika, duka la dawa Mkomaindo, Soko la Tandale na ushuru wa meza ndogo.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.