Kamati ya Fedha na Utawala Halmashauri ya Mji Masasi Oktoba 27, 2023 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kamati hiyo imetembelea na kukagua miradi inayotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali kuu na fedha kupitia mradi wa SEQUIP ambao ni mradi wa uboreshaji wa elimu ya sekondari wenye lengo la kuhakikisha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji yanaboreshwa katika shule za sekondari.
Kamati imetembelea, Ujenzi wa nyumba 1 kwa 2 ya walimu shule ya Sekondari ya kutwa Temeke - Masasi unaotekelezwa kwa fedha za Sequip kwa gharama ya Tsh. 95,000,000.
Kamati pia imekagua Ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Jida unaotekelezwa kwa fedha za Sequip kwa gharama ya Tsh. 560,552,872.
Aidha wametembelea na kukagua, Ukamilisha wa Ujenzi wa Zahanati ya Napupa unaotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu kwa gharama ya Tsh. 50,000,000.
Ujenzi wa Vyumba 9 vya madarasa na Matundu 16 ya vyoo vya Shule ya Msingi Mkomaindo unaotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu kiasi cha Tsh. 208,000,000.
Ukamilishaji wa Ujenzi wa Zahanati ya Matawale unaotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu kwa gharama ya Tsh. 150,000,000.
Pia imetembelea na kukagua Ujenzi wa Bwalo, Madarasa na Vyoo shule ya Sekondari Mwengemtapika unaotekelezwa na fedha kutoka Serikali Kuu kwa gharama ya Tsh 320,000,000.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi Mhe. Hashim Namtumba na wajumbe imeridhishwa na Utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaosimamiwa na watalaamu chini ya Mkurugenzi wa Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu sambamba na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoka fedha za utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji Masasi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.