Kamati ya fedha na Utawala Halmashauri ya Mji Masasi Januari 25, 2024 imetembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kamati hiyo imeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe, Hamisi Nikwanya akimwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi.
Kamati hiyo imetembelea na kukagua Ujenzi wa vyumba vya madarasa, Matundu ya vyoo na bwalo Shule ya Sekondari Mwengemtapika, Ujenzi wa Jengo la upasuaji hospitali ya Mkomaindo, Jengo la Mama na Mtoto Hospitali ya Mkomaindo, shule mpya ya Msingi Darajani, shule ya msingi mkomaindo na shule mpya ya sekondari Jida.
Kamati pia imekagua Ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Jida unaotekelezwa kwa fedha za Sequip kwa gharama ya Tsh. 560,552,872.
Ujenzi wa Vyumba 9 vya madarasa na Matundu 16 ya vyoo vya Shule ya Msingi Mkomaindo unaotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu kiasi cha Tsh. 208,000,000.
Pia imetembelea na kukagua Ujenzi wa Bwalo, Madarasa na Vyoo shule ya Sekondari Mwengemtapika unaotekelezwa na fedha kutoka Serikali Kuu kwa gharama ya Tsh 320,000,000.
Kamati hiyo imepongeza juhudi za Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini, Mhe. Geoffrey Mwambe kwa jitihada za kuhakikisha miradi inawafikia wananchi wa Masasi Mji sambamba na kutoa shukurani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.