Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu amesema ziara ya ugeni wa marafiki wa Masasi kutoka wilaya ya Enzkreis ya nchini Ujerumani ni ishara ya kuendelea kuimarisha uhusiano huo wa muda mrefu uliopo kati ya Masasi na Enzkreis katika nyanja mbalimbali ikiwemo Afya, Mazingira hususani kuongeza ushirikiano katika suala la udhibiti taka , elimu, ujuzi na kubadilishana uzoefu kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Masasi.
Amebainisha hayo katika hafla ya kuwakaribisha wageni hao akiwemo Bi. Angela Gewiese mratibu wa miradi ya ushirikiano Enzkreis na Masasi, Daktari bingwa Dr. Nils Herter kutoka hospitali ya Enzkreis ujerumani, Ulrich Klotz, Afisa Muhifadhi Misitu kutoka ofisi ya misitu ya Enzkreis, na Daktari bingwa wa mifupa Dr. Lunemo Sakafu kutoka Mbeya Refferal Hospital katika (welcome dinner) iliyofanyika katika mgahawa uliopo kituo cha elimu ya mazingira Novemba 24, 2025.
Katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Ndg. Jichabu alisema,
“Ziara yenu ni ishara ya kuendelea kuimarisha uhusiano huu wa muda mrefu uliopo kati ya Masasi na Enzkreis katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Afya, Mazingira, elimu, ujuzi na kubadilishana uzoefu, lakini pia ni matarajio yetu kwamba tutaongeza ushirikiano zaidi katika suala la udhibiti wa taka, ni suala muhimu sana nadhani mtapata muda wa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo dampo letu, mtajionea wenyewe lakini pia nashukuru ujio wa madaktari bingwa wa mifupa kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu hospitali ya Mkomaindo na kubadilishana uzoefu na madaktari wa Masasi”

Wilaya ya Enzkreis ya Nchini Ujerumani, Halmashauri ya Mji Masasi, Halmashauri ya Wilaya Masasi, TAREA na TFS wanaendelea kushirikiana kwa pamoja kupitia miradi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Masasi.
Kwa pamoja wanatekeleza mradi wa NAKOPA kwa mwaka wa fedha 2025/2026 mpaka mwisho wa mwaka 2027.
Mradi huo wenye jina la Shule za kijani, upandaji miti, uvunaji wa maji na elimu ya Mazingira kwa ajili ya Maendeleo endelevu Masasi, Unalenga kuboresha mazingira, kuongeza upatikanaji wa maji mashuleni, elimu juu ya nishati mbadala na nishati safi ya kupikia na kuimarisha elimu ya uhifadhi mazingira kwa wanafunzi na jamii ya Masasi kwa ujumla.





MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.