Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Masasi Mji
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bw. Elias Ntiruhungwa amekabidhi vyumba 37 vya madarasa vilivyokuwa vinajengwa chini ya programu ya Maendeleo ya Jamii na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Brig. Jen. Marco Elisha Gaguti leo tarehe 10/12/2021.
Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika Shule ya Sekondari ya wasichana Masasi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mtwara pamoja na Wilaya ya Masasi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Claudia Kitta.
Mhe.Brig. Jen. Gaguti ametoa pongezi kwa Mkurugenzi na wataalam wote wa Mji Masasi kwa kusimamia ujenzi na kukamilisha ndani ya muda uliopangwa na kueleza kuwa ameridhishwa na jinsi mradi ulivyotekelezwa.
Aidha Mhe. Brig.Jen. Gaguti amesisititiza wanafunzi na walimu kutunza miundombinu ya vyumba hivyo kwani vimejengwa kwa gharama kubwa. Pia Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wazazi kuendelea kutoa chakula kwa wanafunzi ili kupunguza mdondoko wa wanafunzi Mkoa wa Mtwara.
Ujenzi wa vyumba vya madarasa Halmashauri ya Mji Masasi ulianza kutekelezwa kuanzia tarehe 25/10/2021 hadi tarehe 09/12/2021.
Halmashauri ya Mji Masasi ilipokea TZS milioni 820 ili kujenga vyumba 37 vya madarasa pamoja na bweni 1 katika shule ya Msingi Masasi kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.