Watumishi na wananchi wa Halmashauri ya Mji ya Masasi Mkoani Mtwara wameadhimisha siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira katika hospitali ya Mkomaindo iliyopo halmashari ya Mji Masasi ikiwa ni moja ya kumbukizi ya mashujaa wa Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kukamilisha shughuli hizo Mkuu wa wilaya ya Masasi Lauter John Kanoni ameeleza kuwa kila julai, 7 ya kila mwaka serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaadhimisha siku ya mashujaa ambao walipigania Taifa letu tangu kipindi cha Mkoloni baada ya uhuru mpaka sasa hivi.
‘’Tumefanya usafi kwa kushirikiana na wananchi nakuwatembelea wagonjwa waliopo katika hospitali hiyo kama agizo la serikali ya jamhuri ya Muungani wa Tanzania’’DC Kanoni.
Maadhimisho ya siku ya Mashujaa hufanyika kila mwaka ifikapo julai 25,ambapo hutoa fursa ya kuwakumbuka Mashujaa wa Tanzania waliojitolea Maisha yao kwa ajili ya kupigania Nchi yetu,maadhimisho hayo kitaifa mwaka 2023 yanafanyika Mkoani.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.