UANZISHWAJI wa shule mpya ya msingi ya mkondo mmoja Mkomaindo iliyopo katika mtaa wa Darajani utapunguza msongamano wa wanafunzi,utoro pamoja na kutembea umbali mrefu wa kwenda shule mama ya awali.
Imeleezwa kuwa baada ya vikao vya kamati mbalimbali ambavyo vilihusisha wananchi waliamua kuwa shule hiyo ijengwe mtaa wa Darajani ili kusogeza huduma za kijamii na hasa ukizingatia kuwa Kata hiyo ina shule moja tu.
Hayo yamesemwa na Mwalimu Mkuu wa shule Mama Mkomaindo ,Suzan Mwaya wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Masasi alipofanya ziara ya kutembelea shule hiyo ambayo imezojengwa kwa mradi wa Boost.
Ambapo ameeleza kuwa shule ya Mkomaindo ilipatiwa zaidi ya mil.331 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya yenye mkondo mmoja
Mwaya amesema kuwa shule hiyo kwasasa ipo kwenye hatua za umaliziaji vimebaki vitu vichache na kwamba walipata changamoto kubwa kwenye matundu ya vyoo vya wanafunzi ya awali kwani walishauriwa kuwa hayako sehemu sahihi ikabidi yafukiwe na kuchimbwa sehemu nyingine.
“Namshukuru sana Rais Samia kwa kutuona hata sisi tuliopo pembezoni mwa Tanzania na kuona matatizo tunayopata kwenye uwezeshaji katika sekta ya elimu ,shule ya msingi Mkomaindo ina wanafunzi wengi ambao ni 1,531 kiasi kwamba unakuta darasa moja wanakaa watoto 185 hivyo kushindwa kumfikia hata yule mtoto aliyemwisho kabisa,”amesema.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.