Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi bi. Erica Yegella julai 27,2023 amefanya kikao na wafanyabiashara wa Soko la Matunda Jida (Tandale) kikao ambacho kimehudhuriwa na wakuu wa Idara , Viongozi wa NMB bank na wafanyabiashara wa Soko hilo lengo la Kikao hicho ni kutoa Elimu ya biashara na mikopo kwa wafanyabiashara ambapo ofisi Mkurugenzi imetoa dhamana kwa wafanyabiashara hao.
Bi. Erica ameeleza kuwa kila mfanyabiashara mwenye kizimba , leseni ya biashara na anaelipa ushuru wa Halmashauri atapewa Mkopo bila "
yule ambaye atakuwa anamiliki kizimba na amelipa ushuru wa Halmashauri na anahitaji Mkopo NMB bank atapewa mkopo bila dhamana ,dhamana yake itakuwa kizimba na leseni ya Halmashauri" Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi bi.Erica Yegella.
Kwa upande wake Meneja wa NMB bank Ndg.Davis Minja amesema kuwa Mikopo ambayo itatolewa itaitwa Mikopo ya Machinga Loan na mikopo hiyo itakuwa na bima ya sh 10,000 bima hiyo itamsaidia pale ambapo wizi utatokea ,Mafuriko NMB watarudisha Mtaji kwa mfanyabiashara.
"Tutarudisha Mtaji wako pale tuu changamoto ya wizi ikitokea ,Mafuriko bank ya NMB tutakupa Mtaji wako "
Wafanyabiashara wa Soko hilo wamemshukuru Mkurugenzi wa Mji Masasi Bi. Erica Yegella kwa kushirikiana na bank ya @nmbtanzania kuwasogezea fursa ya mikopo nafuu ambayo haina Masharti Makubwa kwani itakuja kuwakomboa katika uendeshaji wa biashara zao.
"Tunamshukuru mama bi.Erica Yegella kwa kutupambania wafanyabiashara wa soko hili kwani mama ni mkombozi wetu ,hii Mikopo itakuja kutuongezea Mitaji yetu tuwe na biashara kubwa ambazo tutapata faida ili kuweza kuendesha Maisha yetu na watoto wetu"wafanyabiashara
Aidha Davis ameeleza kuwa bank ya NMB ipo kwa ajili ya kuwakomboa wananchi na inagusa nyanja zote ambazo watu wengi watakuwepo kama vile Elimu pamoja Mazingira.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.