Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Lauteri John Kanoni amewapongeza wakazi wa Kijiji cha Makulani na wananchi wa Halmashauri ya Mji Masasi kwa ujumla kwa kutimiza wajibu wa kuwapeleka watoto wao shule kwa ajili ya kuanza kidato cha kwanza mwaka 2025 ikiwa ni matunda ya mikakati madhubuti ikiwemo mkataba na wazazi wa kuwapeleka watoto shule.
Mhe. Kanoni ametoa pongezi hizo Machi 21, 2025 katika mkutano na wananchi wa Kijiji cha Makulani ikiwa ni muendelezo wa kliniki za kusikilizaa na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Kanoni amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Makulani na Halmashauri ya Mji Masasi kwa ujumla kwa jitihada walizozifanya kuhakikisha kuwa wanafunzi waliofaulu kwenda kidato cha kwanza wanaripoti shule walizopangiwa kwani Elimu ni kipaumbele namba moja.
‘’Mpaka sasa wanafunzi 2105 kati ya wanafunzi 2107 wamesharipoti katika shule walizopangiwa kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza’’ aliongeza Dc Kanoni.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Sululu Mhe. Rashid Liundi amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwatembelea kwa ajili ya kutatua changamoto zao , mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mhe. Geoffrey Mwambe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto za madarasa, zahanati na uhaba wa madawati katika kata hiyo.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.