Katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru 9 Disemba 2022 ,Mkuu wa wilaya ya Masasi Claudia Kitta , katibu Tawala ,pamoja na viongozi mbalimbali wameungana na wananchi wa halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara kufanya Usafi wa Mazingira katika Maeneo ya vituo vya afya,Sokoni ,Stend za Mabasi .
Katika Zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Masasi wamewataka wananchi wote kuwa wazalendo na kujitkeza kwa wingi kushiriki Kongamano la kuhitimisha kilele cha maadhimisho hayo ambalo litafanyia katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya wasichana Masasi siku ya tarehe 9 ,Disemba 2022.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru kwa mwaka 2022 ni ‘Miaka 61 ya Uhuru Amani na Umoja ni Nguzo ya Maendeleo’
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.