Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bi Claudia Kitta amewapongeza wazazi na walezi wa Vijana ambao wamehitimu Mafunzo ya Jeshi la akiba (MGAMBO) Kwa kuwawezesha Vijana wao kujiandikisha na Jeshi Hilo kwani ni Moja ya Uzalendo waliuonyesha Kwa Serikali.Ameyasema hayo December 8 katika Hafla ya ufungaji Jeshi Hilo uliofanyika katika Kijiji Cha Mkarakate kata ya Sululu Halmashauri ya Mji Masasi.
Aidha amewaomba Vijana wote walohitimu kwenda kuonyesha Uzalendo na Kutoa ushirikiano Kwa jamii katika kuilinda Masasi na Taifa kiujumla pale Changamoto za Usalama zinapotokea.Aidha amewashukuru wakufunzi Kwa Kutoa Maarifa na kuwapa Vijana hao kwani anaimani Vijana wote wamepata Elimu Bora na wataenda kuwa Raia wema.
Jeshi la akiba lililofanyika Kijiji Cha Mkarakate kata ya Sululu limeanza Julai 11.2022 likiwa na Jumla ya Vijana 107 kati yao wanaume 89 ,Wanawake 18 na Vijana 14 waliacha Mafunzo hayo kutokana na Changamoto mbalimbali ikiwemo Ugonjwa na utovu wa nidhamu na kumalizika December 8 2022 likiwa na Vijana 93.
Kwa upande wao Vijana ambao wamehitimu Mafunzo wametoa ombi Kwa Serikali kuwafikiria pale Nafasi za Ajira zinapotoka wapewe kipaumbele.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.