Benk ya CRDB Kanda ya kusini wamekabidhi Meza 50 na Viti 50 vyenye thamani ya shilingi milioni 3.5 kwa Mkurugenzi wa Mji Masasi Bi.Erica Yegella .
Makabidhiano hayo yamefanyika Agost 2,2023 ikiwa ni sehemu ya Mchango wa benk hiyo katika kusaidia jamii kwenye sekta ya Elimu katika shule za Sekondari.
Kwa upande wake Meneja wa bank ya CRDB Kanda ya Kusini Ndugu Denis Mwoleko amesema kuwa benk ya CRDB inaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Samia Suluhu Hassani katika kuleta mapinduzi ya Elimu kwa kutumia faida ya asilimia 1 .
Aidha Meneja wa Tawi Masasi Bi.Herieth Rwechungura amesema kuwa utoaji wawa viti na Meza ni kuunga mkono jitihada za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Mkurugenzi Mji Masasi bi.Erica Yegella ameishukuru benk ya CRDB kwa mchango wao na kuwa karibu na jamii ambao mchango wao umeenda kugusa jamii na kucochea maendeleo ya Elimu katika shule za Masasi Mji.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.