Watumishi wa Halmashauri ya Mji Masasi September,03,2024 wamepata Elimu ya Utambuzi wa Noti na Utunzaji wake Sambamba na utambuzi wa Noti bandia.
Akizungumza na watumishi katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Meneja Huduma za kibenki kutoka Tawi la Benki Kuu Mtwara Ndg, M.D. Rutayebesibwa amesema Benki ya Tanzania inatoa mara kwa mara elimu kwa umma kuhusu elimu ya alama za usalama zilizopo kwenye noti ya benki kuu ili kujiepusha na matatizo ya kupokea noti bandia na utunzaji mzuri wa noti zinazotolewa ili kuondoa tatizo la uharibifu wa noti.
Amesema kazi mbalimbali za Benki kuu ya Tanzania ni pamoja na Kutengeneza fedha, Kusambaza na kuondosha pesa zote zilizochakaa kwenye mzunguko, sambamba na kueleza njia za utambuzi wa noti bandia ambazo ni kwa njia ya Kuona kwa Macho, Hisia kwa walemavu wa Macho na kupitia taa za mwanga wa bluu ambao unasadia kuakisi namba zilizomo pembezoni mwa Noti.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg.Reuben Sixbert Jichabu ameishukuru Benki Kuu ya Tanzania kwa kutoa elimu hiyo na kwamba inakwenda kuwasaidia watumishi katika utambuzi na utunzaji wa noti.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.