Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Masasi chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Hashim Namtumba April 30, 2024 limepokea, kujadili na kupitisha taarifa za kata robo ya tatu, 2023/2024 katika mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Jengo la Utawala.
Baraza hilo limepokea, kujadili na kupitisha Taarifa za kata ya Chanikanguo, Jida, Migongo, Mkomaindo, Mkuti, Temeke, Mumbaka, MwengeMtapika, Napupa, Nyasa, Sululu, Mtandi, Marika na Matawale.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa Baraza hilo, waheshimiwa madiwani wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji Masasi.
Waheshimiwa wamezungumza kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji, umeme, elimu na miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali ya Mji.
Aidha, limempongeza Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mhe. Geoffrey Mwambe kwa jitihada zake za kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unawafikia wananchi wa Kata zote 14 za Halmashauri ya Mji Masasi.
Baraza hilo, limempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu kwa kasi yake ya kusimamia vyema na kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati, ufanisi, ubora na kutumika kwa wakati.
Baraza hilo limehudhuriwa na waheshimiwa madiwani, watendaji wa kata, vyama vya siasa, wazee maarufu, wakuu wa Idara na vitengo.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.