Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Masasi agost 28, 2022 limeketi kwa ajili ya kupitia taarifa ya hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha 2021/2022 wakati huo mwaka wa fedha 2020/2021 halmashauri ya Mji Masasi ilipata hati Safi na huu ni mwendelezo wa miaka mitatu mfululizo halmashauri ikiwa na hati safi.{Unqualifief Opinion}
Akiwasilisha taarifa hiyo mweka hazina wa halmashauri ya Mji Masasi Donasian Mgozi amesema kuwa kwa Mujibu wa kifungu cha 31{1}cha Demoranda ya fedha za serikali ya mitaa inaeleza kuwa hesabu za mwisho za halmashauri ziandikwe vizuri na kuwasilishwa kwenye mkutano wa baraza la madiwani na baadae ziwasilishwe kwa mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali {CAG} ndani ya miezi mitatu baada ya mwisho wa mwaka.
Mweka hazina ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2021/2022 taarifa ya Mizania ya hesabu inaonyesha kuwa halmashuri ya Mji Masasi ilikuwa na Mali za kudumu zenye thamani ya sh.25,245,525,061.00 ikilinganishwa na sh.22,083,362,023.00 zilizokuwepo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na hiyo ni ongezeko la asilimia 14.3 iliyotokana na kukamilika kwa jingo la utawala ,nyumbatano za watumishi na majengo ya hospitali ya mji masasi Mkomaindo na Soko la Tandale.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.