Halmashauri ya Kijiji itakuwa na wajumbe wasiozidi ishirini na tano watakaochaguliwa na wakazi wa vitongoji katika kijiji kama ifuatavyo:
(a) Mwenyekiti wa Kijiji;
(b) Wenyeviti wa vitongoji vilivyomo katika eneo la kijiji;
(c) Wajumbe mchanganyiko wanawake na wanaume; na
(d) Wajumbe wa kundi la wanawake ambao idadi yao haitakuwa chini ya theluthi moja ya wajumbe wote wa Halmashauri ya kijiji.
12.2 Kamati ya Mtaa itakuwa na wajumbe wasiozidi sita watakaochaguliwa na wakazi wa mtaa. Wajumbe
hao ni wafuatao:-
(a) Mwenyekiti wa Mtaa;
(b) Wajumbe wengine watano ambao kati yao wajumbe wasiopungua wawili watakuwa wanawake.
12.3 Wenyeviti wa vitongoji watakaochaguliwa kutoka kila kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.