Mkuu wa wilaya ya Masasi Lauter John Kanoni ametoa pongezi kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo anaifanya ya kutoa Fedha za Utekelezaji wa Miundo ya ujenzi wa Shule za Msingi.
Kanoni ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani la kupokea taarifa za kamati na kuzijadili Halmashauri ya Mji Masasi kilichoketi May 6,2023 katika Uikumbi wa Mikutano ,kikao ambacho kilihudhuriwa na Madiwani,wakuu wa Idara na Vitengo ,kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya.
Aidha Kanoni amewaomba Madiwani wote kwa kushirikiana na wataalamu waliopo Halmashauri kusimamia Fedha ambazo zinaletwa kwa lengo la kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo iliyopo katika Halmashauri ili kufikia Malengo mahususi ya Serikali.
Kanoni ameeleza kuwa Halmashauri ya Mji Masasi imepokea Fedha Shilingi Milioni miasita themanini na mbili na laki tatu (682,300,000.00) kutoka Mradi wa Boost kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa Miundo mbinu ya Shule za Msingi.
Kutokana na fedha hizo amewaomba wataalamu kuzitumia vizuri fedha hizo ili kukamilisha Ujenzi wa Miundo ya shule kwa wakati hadi kufikia June 26,2023 iwe imekamilika ili Serikali iweze kutoa fedha zingine.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Elias Ntiruhungwa ameahidi kusimamia vema fedha hizo na kuhakikisha Miradi inakamilika kwa wakati kama agizo lilivotolewa.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.