Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu amewaasa Maafisa Bajeti kuhakikisha wanazingatia vipaumbele na uhalisia katika maandalizi ya bajeti ili kuboresha utekelezaji wa miradi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa ufanisi.
Ameyasema hayo Novemba 27, 2025 wakati wa mafunzo kwa wakuu wa Idara na Vitengo na Maafisa bajeti wa Halmashauri yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri yakilenga kuwajengea uwezo Maafisa Bajeti ili waweze kuandaa na kusimamia mipango ya fedha kwa usahihi, uwazi na ufanisi.
Aidha amesema kuwa ni muhimu bajeti kuandaliwa kwa kuzingatia hali halisi ya mahitaji, vipaumbele vya wananchi na miongozo ya Serikali, ili kuepuka upangaji wa shughuli ambazo hazitekelezeki kutokana na ukosefu wa rasilimali.

Naye, mratibu wa mafunzo hayo na Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu, Ndg. Petro Marwa amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu katika kuhakikisha maandalizi ya bajeti yanafanyika kwa ufanisi na kwa kuzingatia miongozo ya Serikali.
Aidha amesisitiza kuwa kupitia mafunzo hayo, washiriki wataweza kuhakikisha rasilimali za Serikali zinapangwa na kutumika ipasavyo kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi sambamba na kuimarisha uwajibikaji na matumizi sahihi ya rasilimali za umma kwa manufaa ya wananchi.







MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.