• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe za Watumishi |
Masasi Town Council
Masasi Town Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisa Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Mji Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha
    • Machapisho
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Biashara
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Utawala na Utumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango miji na mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Makataba ya Picha

“MIRADI HII NI MKOMBOZI KWA WANANACHI WOTE WA MASASI” DC KANONI.

Posted on: February 25th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Lauteri John Kanoni leo Februari 25, 2025 amezungumza na mamia ya wananchi na wafanyabiashara wa Wilaya ya Masasi katika Soko la Mkuti Halmashauri ya Mji Masasi ambapo ameeleza kuhusu mafanikio mbalimbali ya Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan sambamba na miradi ya kimkakati inayotarajiwa kutekelezwa Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara. 

Mhe Kanoni amesema miongoni mwa miradi ya kimkakati ambayo inatarajiwa kutekelezwa ni Miradi ya TACTICS ambayo ina lengo la kuboresha miundombinu katika miji mbalimbali na inafadhiliwa na Benki ya dunia.

Amesema katika miradi hiyo Masasi imepata bahati ya kipekee ambapo kwa  Halmashauri ya Mji Masasi ipo katika Kundi la tatu ikiwa ni pamoja na halmashauri za miji ya Bunda TC, Handeni TC, Ifakara TC, Kasulu TC, Kondoa TC, Mafinga TC, Makambako TC, Masasi TC, Mbinga TC, Mbulu DC, Nanyamba TC, Newala TC, Nzega TC, Tarime TC, Tunduma TC, Vwawa TC, Bagamovo DC, Chato DC.

Mhe Kanoni amesema kuwa Halmashauri ya Mji wa Masasi ikiwa kama wanufaika wa mradi huo wa TACTICS kupitia kundi la tatu imefanikiwa kupata miradi mitatu ambayo ni barabara zenye urefu wa kilometa 5.67 kwa kiwango cha lami ambazo ni adam viazi road, NMB anglican road, Makaburini road, Mtandi mission road, Napupa Mkuti road, Mpunga road na Masai Navai road  ambazo zitachochea ukuaji wa Mji na kupendezesha Mji na kupunguza  msongamano wa magari katikati ya Mji.

Amesema mradi mwingine ni ujenzi wa  Stendi ya kisasa katika eneo lenye ukubwa wa hekta 5.0412 lililopo eneo la Tokura kata ya Mwenge Mtapika ambao utasaidia kuongeza wigo wa biashara ya usafiri, Kuongeza wigo wa kibiashara kutoka mikoa Jirani, Mazingira rafiki na salama ya kufanyia Biashara na Kuimarika kwa ulinzi na usalama wa mali.

Amesema mradi wa tatu ni mradi wa ujenzi wa soko la kisasa katika  Halmashauri ya Mji wa Masasi katika eneo la Mkuti lenye ukubwa wa 4412m2 lilipo eneo la Mkuti kati kata ya Mkuti ambao una faida za kuongeza upatikanaji huduma kwa wanachi, Kufanya biashara katika mazingira rafiki na salama, Kutanua wigo wa kibiashara, Kuongeza mapato ya wafanyabiashara na Kuimarika kwa ulinzi na usalama wa mali.

Wakizungumza katika mkutano huo, Wananchi na wafanyabiashara wamesema wapo tayari kwa utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuwa itakwenda kuinua Uchumi wa wananchi na Masasi yote kwa ujumla na kuongeza wigo wa ajira kwa wananchi. 

 

 

 

 

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 28, 2020
  • TANGAZO LA KAZI April 05, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • Kuona Vyote

Habari Mpya

  • “VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA MKOA WA MTWARA TUWEKE KIPAUMBELE CHA UTOAJI WA HUDUMA ZA TIBA OKOVU NA HUDUMA MSINGI KWA WAGONJWA MAHUTUTI” RAS MTWARA.

    May 15, 2025
  • “WANANCHI TUJITOKEZE MKOMAINDO HOSPITALI KUPATA VIPIMO NA MATIBABU YA SARATANI BURE, SERIKALI IMELIPIA GHARAMA (SAMIA SULUHU OUTREACH SERVICES)” DC KASSANDA

    April 23, 2025
  • HISTORIA YAANDIKWA MASASI MJI, ZAIDI YA MILIONI 545 ZATOLEWA MWAKA HUU WA FEDHA 204/2025 KWA VIKUNDI 105 MIKOPO YA ASILIMIA 10.

    April 07, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA MASASI MJI WATOA ELIMU KUHUSU TAHADHARI YA UGONJWA WA MPOX

    April 06, 2025
  • Kuona Vyote

Video

SHERIA ZA MITANDAO
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Sheria ndogo ya Ada na Ushuru kwa Mji wa Masasi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Mtwara
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais UTUMISHI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • SALARY SLIPS PORTAL

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MASASI TOWN COUNCIL

    Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI

    Simu Ya Mezani: +255 23 2510685

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: info@masasitc.go.tz

Mawasiliano

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma Zetu

Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.