Idara ya Utawala na Utumishi katika Halmashauri ya Mji Masasi ina jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa malengo ya Halmashauri ya Mji yanafikiwa kwa kusimamia vema rasilimali watu iliyopo kwa mujibu wa Sheria, Kanuni , Taratibu pamoja na miongozo mbalimbali inayotolewa. Lengo la usimamizi wa Rasilimali watu/watumishi ni kuweka utaratibu wa utendaji kazi katika Utumishi wa Umma ili kuhakikisha kuwa maadili ya Utumishi wa Umma yanafuatwa ipasavyo katika kutoa huduma iliyo bora na kwa wakati kwa wananchi wanaowategemea. Huduma zinazotolewa na Idara hii ni pamoja na:
Huduma ya Dawati la Malalmiko
Huduma ya Dawati la Huduma kwa Mteja
Huduma ya bUsafiri na Usafirishaji
Usimamizi wa Maslahi ya Watumishi Wote na Waheshimiwa Madiwani