• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe za Watumishi |
Masasi Town Council
Masasi Town Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisa Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Mji Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha
    • Machapisho
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Biashara
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Utawala na Utumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango miji na mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Makataba ya Picha

BARAZA LA MADIWANI MJI MASASI LIMERIDHIA NA KUPITISHA BAJETI YA BILIONI 30 KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025.

Posted on: February 29th, 2024

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Masasi limejadili na kuidhinisha rasimu ya mapendezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2024/2025  ambapo Halmashauri hiyo inakadiria kupokea na kutumia jumla ya Tsh. 30,195,139,106.07.

Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili na kupitisha bajeti hiyo Februari 29, 2024, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi Mhe. Hashim Namtumba amesema  bajeti hiyo imezingatia mapendezo yote muhimu ya waheshimiwa madiwani na hivyo itakwenda kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mhe, Geoffrey Mwambe amesema bajeti hiyo imezingatia vipaumbele vya wananchi wa Masasi Mji.

Amesema mbali na bajeti hiyo bado anaendelea kupambana kwa dhati kuhakikisha ujenzi wa masasi mpya unawafikia wananchi wa Masasi Mji katika kata zote 14 kupitia uboreshaji wa miundombinu ambapo barabara ya kisasa yenye miradi funganishi kama stendi ya kisasa inakwenda kujengwa sambamba na maboresho ya kisasa katika standi ya uwanja wa fisi (ambayo ameshauri maboresho yakishafanywa jina libadilishwe), sambamba na ujenzi na maboresho katika eneo la Sokosela.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu amesema katika jitihada za kuongeza mapato ya ndani, katika mwaka wa fedha 2024/2025 wanatarajia kujenga hoteli ya kisasa yenye kumbi kubwa tatu za mikutano na kumbi ya starehe sambamba na kuboresha miundombinu ya shule, kuwezesha wananchi kiuchumi,kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya.

Akiwasilisha rasimu ya bajeti hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mji, Mkuu wa divisheni ya Mipango na Uratibu Halmashauri ya Mji Masasi, Ndg. Prosper Luambano amesema Halmashauri inakadiria kupokea na kutumia jumla ya shilingi 30,195,139,106.07 kutoka katika vyanzo mbalimbali.

Amesema vyanzo hivyo ni mapato ya ndani shilingi 3,397,212,700.00, matumizi mengineyo shilingi  1,040,957,000.00, Mishahara-shilingi 18,764,926,000.00, Miradi ya maendeleo (Serikali kuu na Wahisani) shilingi  6,992,043,406.07

Amesema vipaumbele vya bajeti hiyo ni kuongeza mapato ya ndani kutoka Tshs 2.8 Billion ya sasa hadi Tshs Billioni 3.4., Kuimarisha shughuli za utawala bora, Kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya, Uimarishaji wa usafi wa mazingira, Kuboresha miundombinu ya shule za Msingi, Uwezeshaji wananchi kiuchumi, Ukamilishaji wa miradi viporo, Umilikishaji wa maeneo ya umma.

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa Mkutano wa kujadili na kuidhinisha rasimu ya mpango wa bajeti Halmashauri ya Mji Masasi kwa mwaka wa fedha 2024/2025



 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 28, 2020
  • TANGAZO LA KAZI April 05, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • Kuona Vyote

Habari Mpya

  • “VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA MKOA WA MTWARA TUWEKE KIPAUMBELE CHA UTOAJI WA HUDUMA ZA TIBA OKOVU NA HUDUMA MSINGI KWA WAGONJWA MAHUTUTI” RAS MTWARA.

    May 15, 2025
  • “WANANCHI TUJITOKEZE MKOMAINDO HOSPITALI KUPATA VIPIMO NA MATIBABU YA SARATANI BURE, SERIKALI IMELIPIA GHARAMA (SAMIA SULUHU OUTREACH SERVICES)” DC KASSANDA

    April 23, 2025
  • HISTORIA YAANDIKWA MASASI MJI, ZAIDI YA MILIONI 545 ZATOLEWA MWAKA HUU WA FEDHA 204/2025 KWA VIKUNDI 105 MIKOPO YA ASILIMIA 10.

    April 07, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA MASASI MJI WATOA ELIMU KUHUSU TAHADHARI YA UGONJWA WA MPOX

    April 06, 2025
  • Kuona Vyote

Video

SHERIA ZA MITANDAO
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Sheria ndogo ya Ada na Ushuru kwa Mji wa Masasi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Mtwara
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais UTUMISHI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • SALARY SLIPS PORTAL

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MASASI TOWN COUNCIL

    Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI

    Simu Ya Mezani: +255 23 2510685

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: info@masasitc.go.tz

Mawasiliano

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma Zetu

Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.