Kamati ya Uchumi ,ELimu na afya halmashauri ya Mji Masasi Oktoba 17,2022 imefanya ziara ya kutembelea Vikundi vya wanawake ,Vijana ,watu wenye ulemavu pamoja na Shule tatu za Msingi Kwa lengo la kukagua na kuona Maendeeleo ya Vikundi ambavyo vimepatiwa Mikopo ya asilimia Kumi Kwa ajili ya kujiendeleza katika shughuli zao za kiuchumi.Katika ziara hiyo Kamati imetembelea Vikundi vitatu ambavyo ni kutandakulewa kikundi Cha watu wenye ulemavu ambacho kinapatikana kata ya Mtandi kinachojishughulisha na shughuli za ufugaji kuku ,Kuuza mitungi ya Gas ,na ufugaji wa Nguruwe,Kikundi Cha vijana ambacho kipo kata ya jida kinachojilikana Kwa Jina la Kazi Iendele ambacho kinajishughulisha na shughuli ya ufyatuaji tofali,na kikundi Cha wanawake ambacho kinajishughulisha na shughuli za ufugaji kuku.
Aidha Kwa upande wa Shule wametembelea Shule ya Msingi Temeke na Nangose Kwa ajili ya kusikiliza Changamoto zinazowakabili na kuona Maendeeleo ya Shule hasa katika viwango vya ufaulu na Juhudi zinazofanyika kuhakikisha ufaulu unapanda Kwa asilimia mia Moja (100).
Kutokana na Changamoto ambazo wameziona Katika kipindi Cha ziara Kwa upande wa Elimu Kama Kamati imependekeza kurudi katika Maeneo hayo kuzungumza na Jamii Kwa ajili ya kuwapa Elimu kuhusu umuhimu wa Elimu na namna ya Mzazi/Mlezi anavotakiwa amtumze na kumlea kwa malezi Bora Mtoto wake kipindi anapokuwa Nyumbani.Hamisi Nikwanya ni Mjumbe Kamati ya Elimu ,Afya na Uchumi Ambaye pia ni Diwani kata ya Mumbaka ametoa agizo Kwa afisa Maendeeleo ya Halmashauri ya Mji Masasi Rashidi Njozi kwenda kutoa Elimu Kwa jamii kuhusu Mikopo ya asilimia Kumi na kuwafundisha namna Bora ya kutafuta Masoko Ili waweze kupata Mafanikio Mazuri ambayo yatawaondolea Changamoto Kwa kipindi Cha marejesho ya Mikopo Yao.
Kwa upande wake mwakilishi wa kikundi Cha vijana kata ya jida ambacho kinajishughulisha na shughuli ya ufyatuaji tofali Josephu Hamisi ametoa pongezi Kwa serikali Kwa kuwapatia mkopo wa shilingi Milioni kumi na Tano (15,000,000) kwani zimewaongezea nguvu katika Mradi huo.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.