Kamati ya fedha na Utawala halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara imetoa agizo kwa wataalam wote ambao wanahusika kusimamia Miradi ya maendeleo kuhakikisha wanasimamia majukumu yao mpaka pale Mradi unapokamilika.
Ameyasema hayo 0ktoba 20,2022 Mwenyeketi wa kamati ya fedha na Utawala Mh: Hashim Namtumba ambae pia ni diwani wa kata ya Jida katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo katika robo ya kwanza kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.
Katika ziara hiyo kamati imetembelea na kukagua Miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa sekondari mpya ya Temeke ,ujenzi wa Jengo la kujifungulia zahanati ya Chisegu,Ujenzi wa OPD na Maabara kituo cha Afya Mtandi ,Ujenzi wa choo Soko la Jida ,Ujenzi wa Vyumba vinne vya Madarasa Shule ya Sekondari Anna Abdalla ,Ujenzi wa Zahanati ya Machombe .
Kupitia ziara hiyo kamati ya fedha ilipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Mji Masasi Elias Ntiruhungwa kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Temeke amesema kuwa Halmashauri ilipokea fedha Shilingi 470,000,000.00 ambayo haikutosha kutekeleza Mradi Wote kulingana na Mchoro wa BOQ ya Mradi hivyo hadi kukamilisha Ujenzi wa Majengo yote yaliyoopo kwenye Mchoro ilihitajika fedha Shilingi 700,000,000.00.
’Baada ya kuona fedha hazitoshi Halmashauri iliamua kuanza ujenzi kwa kujenga Majengo ambayo yataweza kupokea wanafunzi na kufanikiwa kujenga jingo la utawala,Vumba 8 vya Madarasa ,Maabara ya kemia na biolojia ,vyoo vya wavulana na Wasichana ambavyo vimekamilika ,na Jengo la Maktaba ambalo bado halijakamilika na tunatarajia kupokea wanafunzi ifikapo januari 2023 kwa sababu shule hii tayar imeshasajiliwa’’Elias Ntiruhungwa.
Baada ya kupokea maelezo hayo kamati imepongeza menejimenti kwa mawazo mazuri ambayo pamoja na Majango kutokamilika kulingana na Mchoro kama ulivokuwa unatakiwa ukamilishwe ila ni hatua ambayo imeleta matumaini yakuweza kutumika pale ifikapo January 2023.
Katika ziara hiyo kamati ya Fedha na Utawala imekagua ujenzo wa jengo la kujifungulia Zahanati ya Chisegu ambapo Mtendaji Kata Zakia Maguno alisoma Taarifa ya Mradi na kueleza vyanzo vya fedha vya Mradi huo kuwa ni Mfuko wa Jimbo ulitoa Shilingi 14,100,000 Nguvu za wananchi Shilingi 500,000 Mfuko wa Afya Shilingi 3,795,000 pamoja na mapato ya Ndani ya halmashauri Shilingi 1,000,000 na Jumla kuu ni Shilingi 19,395,000 ambayo imeweza kukamilisha Mradi huo.
Kamati imepokea taarifa hiyo na kuridhia kwani Maendeleo ya Mradi ni Mazuri yanaonekana na Thamani ya fedha iliyotumika ni sahihi pia wametoa Shukrani kwa halmashauri ya Mji Masasi kwa kuwawezesha kukamilika kwa Mradi huo ambao ni msaada mkubwa kwa wakazi wa kata hiyo.
Vilevile kamati ilifanya ziara katika ujenzi wa zahanati ya Machombe ambapo wajumbe walishuhudia juhudi zilizofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi wa kata hiyo ambapo Mradi huo utagharimu kiasi cha fedha shilingi 106,776,692.00 mpaka kukamilika na hadi sasa Mradi umepokea Fedha shilingi 62,000,000 ikiwa mradi upo hatua ya uchapiaji.
Hivyo kamati imeridhishwa na mradi huo baada ya kukaguwa na wametoa pongezi kwa wasimamizi wa Mradi huo pia kamati imeshauri zifuatwe taratibu zote za manunuzi ili kuepuka hoja za kiukaguzi.
pia wametoa agizo kwa Mhandisi wa halmashauri ya Mji Ombeni Usiri kuandaa BOQ kwa ajili ya ujenzi wa choo ambayo itatumika baada ya kunza kutoa huduma katika zahanati hiyo.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.