Jumla ya watoto elf kumi na saba mia tisa na tatu {17903}halmashauri ya mji Masasi wanatarajia kupata chanjo ya polio katika kampeni ya kitaifa ya awamu ya tatu ambayo inatarajia kuanza September 1,2022 na kumalizika September 4,2022.
Mratibu wa chanjo halmashauri ya wilaya ya Masasi Josephu Stanley Njuyuwi amesema kuwa chanjo hiyo itatolewa kawa kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano {5}ambao waliowahi kupata chanjo zilizopita na wasiopata kabisa.
Ameeleza hayo katika kikao cha kamati ya chanjo ya msingi wilaya ya Masasi kilichofanyika agost 31,2022 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Masasi .
Josephu Stanley ametolea ufafanuzi kwa kampeni ya chanjo iliyopita ya awamu ya pili ambayo ilifanyika Mei 8,2022 hadi Mei 21,2022 amesema kuwa Halmashauri ya Mji Masasi ililenga kutoa chanjo ya polio 13796 ,idadi ya chanjo zilizotumika ni 19480 na idadi ya watoto waliochanja ni 17903 sawa na asilimia 129 hali ambayo imepelekea halmashauri ya Mji kushika nafasi ya pili kati ya halmashauri tisa zilizopo Mkoa wa Mtwara.
Pia amesema chanjo ya Polio ya awamu ya tatu kamati imejipanga vizuri imeongeza timu ambayo itapita nyumba hadi nyumba na maeneo yote ambayo yametengwa kwa ajili ya kutolea huduma hiyo na kuhakikisha kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano anapata chanjo.
Mkuu wa wilaya ya Masasi Claudia kitta ametoa wito kwa wazazi na walezi wote khakikisha wanawapeleka watoto wao kwenda kupata chanjo ya polio katika maeneo yaliyotengwa yakutolea huduma ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali ambayo ni rahisi kwa motto kuambukizwa.
Mwita Leornad Werema ni Mzee maarufu ambaye amehudhuria kikoa hiko ameiomba kamati ya afya yamsingi wilaya ya chanjo ya Polio kutoa Elimu kwa jamii kuhusu faida ya chanjo na hasara ya kutompa Mtoto chanjo ili kuleta hamasa watu wajitokeze ili tufikie malengo.
Kampeni ya chanjo ya polio ya awamu ya tatu itaanza September 1,2022 na kumalizika September 4,2022 kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.