Mkuu wa Wilaya ya Masasi iliyopo Mkoani Mtwara Mh.Claudia Kitta amesema kuwa ni lazima Walimu watambue wajibu wao wa kuhakikisha wanatekeleza shughuli ipasavyo katika suala zima la utoaji wa elimu kwa kufuata ratiba za muda wa masomo ya kipindi,kuwajibika na kujiandaa na kuwa wabunifu katika ufundishaji na kuzalisha wahitimu wenye maarifa.
Mh. Kitta ameyasema hayo katika mafunzo ya siku tatu yanayotolewa na ADEM ambayo yanafanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya wasichana Masasi [Masasi Girls] ambapo yameudhuriwa na Maafisa Elimu kata,Walimu wakuu wa shule za Msingi na Sekondari.
‘’mafunzo hayo yakwenda kuwaongezea umahiri katika uongozi, kusimamia, kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kutoa huduma ya elimu vile inavyopaswakwa kufuata miongozo inayotolewa na kwamba pamoja na miongozo hiyo bado yamekuwa yakihitaji kupata mafunzo kama hayo ili kuboresha utendaji kazi’’Alisisitiza Kitta.
Alfonce Amuri ambaye ni Naibu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ADEM amesema lengo la kuendesha mafunzo hayo ni kujenga uelewa kwa Walimu wakuu pamoja na Maafisa Elimu Kata ili kuimarika katika usimamizi wa Rasilimali za shule.‘’nia ya Serikali ni kuendelea kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu katika taasisi za elimu ikiwemo Shule za Msingi na Sekondari kama ilivyofanya’’ Alisema Amuri.
Na kwa upande wa walimu pamoja Maafisa Elimu Kata kutoka Wilaya ya Nanyumbu,Masasi Tc na Masasi Dc wameeleza kufurahishwa kwao na mpango wa Serekali ya Mkoa wa Mtwara kwa kuandaa mafunzo kutoka Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ADEM na kueleza kwamba watakwenda kuyafanyia kazi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.