Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mhe.Geoffrey Mwambe amewaomba wananchi wote wa Jimbo la Masasi Mjini kuunganishiwa huduma ya umeme ili Tanesco wajuwe kuwa wanawateja wengi kwa maeneo ya vijijini.
“Natamani kila mwananchi wa jimbo langu aunganishiwe huduma ya umeme ili Tanesco wajuwe kuwa wanawateja wengi ili mapato yao yaongezeke yawe yakutosha na wao waweze kuhudumia Miundombinu ya Serikali ambayo imewekwa”Mwambe
Aidha Mwambe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan kwa kuongeza Nguzo 40 za umeme kwa kila kijiji kilichopo Jimbo la Masasi Mji kwani ni bahati kubwa saana kwa wananchi wa Masasi.
“kwanza wananchi wangu tunabahati saana Mhe.Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongeza nguzo 40 kwa kila kijiji ili kuhakikisha huduma ya umeme inawafikia wananchi wote” Mwambe
Ameyasema hayo septemba 22,2023 katika kijiji cha Namikunda kata ya Mumbaka halmashauri ya Mji Masasi katika hafla ya Naibu waziri wa Nishati mhe.Judith Kapinga ya kuwasha umeme vijijini kupitia Mradi wa REA 111
Kwa upande wake Naibu waziri wa Nishati Mhe.Judithi Kapinga ameeleza kuwa Mkoa wa Serikali imetoa Billion 98 kwa ajili ya kusambaza umeme Halmashauri zote tisa (9) na Halmashauri ya Mji Masasi wametumia zaidi ya billion 1 na Mkandarasi yuko saiti.
“Serikali imetumia zaidi ya billion 1 kwa na Mkandarasi yuko saiti na lengo letu Masasi Mji tunaenda kuunganisha na Gridi ya Taifa ,tunamshukuru Mhe. Rais na tunategemea ndani ya miezi 18 mpango huu utakuwa umekamilika hivyo natoa rai ya wananchi kuwa na muamko wa kuvuta Nishati hii katika Nyumba zao”Mhe Judith.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.