Walimu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Mji Masasi wanaofundisha kidato cha kwanza mkondo wa jumla na kidato cha pili mkondo wa Amali (masomo ya jumla) leo Januari 6, 2025 wamepatiwa mafunzo kupitia Darasa Janja “Smart Classes”kuhusu utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ulioboreshwa wa mwaka 2023.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanayotolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI yanalenga kukuza uelewa wa jumla kwa walimu kuhusu maboresho ya Mtaala wa Elimu ya Sekondari hatua ya chini kwa Mkondo wa jumla na Mkondo wa Amali na namna ya kutekeleza.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwezesha walimu kumudu mbinu za ufundishaji na ujifunzaji zinazozingatia ujenzi na umahiri.
Kwa Halmashauri ya Mji Masasi mafunzo hayo yanafanyika kuanzia Januari 6, 2025 hadi Januari 8, 2025 katika Ukumbi wa Shule ya Wasichana Masasi huku mtaala huo unatarajia kuanza kutekelezwa Januari 2025.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.