Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wamepongeza ubora wa miundombinu na vifaa tiba vya kutolea huduma za afya katika kituo cha afya Mtandi, Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara.
Aidha wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mhe. Geoffrey Mwambe kwa kupambana kwa nguvu kuhakikisha miradi mbalimbali ikiwemo kituo hicho inawafikia wananchi wote wa Masasi.
Pongezi hizo zimetolewa Novemba 13, 2023 mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Dennis Londo kutembelea na kukagua miundombinu katika kituo cha afya Mtandi.
Mjumbe wa Kamati hiyo, Mbunge Mwita Waitara amesema vifaa tiba katika kituo hicho vina ubora mkubwa na vya kisasa.
" Mhe Mwenyekiti, Hapa wana mitambo ya kisasa kabisa, hapa tumepita Dental service inayotolewa hapa, kwangu kule sijaiona, hivyo nimepiga picha nikawaoneshe wenzangu kwamba kule Masasi, Mtwara Kuchelee..sasa hii kazi ya Mama Samia lazima tuiseme, wananchi wajue kwamba hapa kuna kituo cha kisasa chenye vifaa vya kisasa" Mjumbe wa Kamati, Mbunge Mwita Waitara.
Naye, Mjumbe wa kamati hiyo, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kituo hicho kinafaa kuwa hospitali.
"Nami niungane na wenzangu wote kuipongeza kabisa Halmashauri ya Mji Masasi na Wilaya kwa kujenga kituo cha afya cha viwango vya hali ya juu, kwasisi wahenga hiki sio kituo cha afya, hii ni hospitali, kwakweli viwango vyake ni vya hospitali, kituo cha afya hiki baada ya miaka 10 au 15 kitakuwa hospitali. rai yangu tujitahidi tujenge uzio" Mjumbe wa Kamati, Profesa Kabudi.
Aidha kwa niaba ya Mwenyekiti, Mjumbe wa kamati hiyo, Mbunge Amandus Chinguile ametoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Rais na Mbunge wa Jimbo hilo.
"Nilete salamu za Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini, Mhe. Geoffrey Mwambe, anafanya kazi nzuri sana, jamani hivi vitu havijileti huku kimiujiza, wako watu wanasema kwa niaba yenu, na huyo mtu ni mbunge wenu, anafanya kazi nzuri sana, anazungumza, anazunguka kwenye ofisi mbalimbali na anauzoefu mkubwa sana, hivi vimeletwa Masasi baada ya Mhe Mbunge kusema Masasi tunashida na kituo cha afya na nyingine nyingi" Mjumbe wa Kamati, Mbunge Chinguile.
Aidha, Mjumbe wa Kamati hiyo, Mbunge Salome Makamba amesema ni vyema kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika na maji katika kituo hicho.
"Ujenzi wa Miundombinu katika kituo hiki upo vizuri sana, nashukuru sana mmefanya vizuri, ni sehemu ya kuigwa mfano, pamoja na hii tuboreshe tuwe na reserve ya maji pia umeme, hospitali hii ina vifaa vya kisasa naipongeza serikali lakini lingine ni muhimu kuwa na daktari wa dharula ambaye anakaa karibu na kituo cha afya " Mjumbe wa kamati, Mbunge Salome Makamba.
Halikadhalika, Mjumbe wa kati hiyo, Mbunge Zuberi Kuchauka ameridhika na hali ya ujenzi wa kituo cha afya Mtandi.
"Mimi niungane na wajumbe wenzangu, kwakweri nimeridhika na hali ya ujenzi wa kituo cha afya hiki, tupo vizuri" Mjumbe wa kamati, Mbunge Zuberi Kuchauka.
Katua nyingine, Mjumbe wa kamati hiyo Chinguile ameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Rais- Tamisemi kwa kazi kubwa ya kuwafikia wananchi wa maeneo yote nchini.
"Na mimi niungane na waheshimiwa wabunge wenzangu kuwapongeza wenzetu Masasi lakini kipekee Mhe. Naibu Waziri Dkt. Festo Dugange, hii kazi kubwa na nzuri mmeifanya katika halmashauri hii, hongereni sana lakini pia ni jukumu letu kulinda miundombinu hii" Mjumbe wa Kamati Mbunge Amandus Chinguile.
Ujenzi wa kituo cha afya Mtandi umegharimu kiasi cha Tsh milioni 500, fedha kutoka Serikali kuu.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.