Wafanyabiashara wa Soko la Mkuti na Tandale Septemba 01,2024 wamempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu na Wataalam wake kwa kuongoza zoezi la Usafi kabambe wa uzoaji taka katika Maeneo ya Soko la Mkuti na Soko la Tandale kwa kutumia Malori zaidi ya manne na Mtambo wa Excavator.
Wakizungumza wakati wa zoezi hilo, wafanyabiashara hao akiwemo Shaban Nyamwelu wamesema zoezi hilo limeondoa Kero ya taka katika maeneo hayo na kwamba ni jukumu la wananchi na wafanyabiashara kuhakikisha taka zinazokusanywa katika maeneo ya Sokoni hazitoki nje na maeneo ya Soko ili Kupunguza mlundikano wa Taka.
Katibu wa Soko Kuu Mkuti , Ndg. Mussa Athuman ametoa wito kwa wafanyabiashara kuzingatia mipaka ya sehemu ya kukusanyia taka na kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi wa mtu mwingine katika kutupa taka kwa usahihi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa Taka na Usafi wa Mazingira Bi. Teresia Ndunguru amesema zoezi hilo limekwenda sambamba na Usafi wa Mwisho wa Mwezi na kwamba zaidi ya Malori Manne na Mtambo mmoja vimetumika kufanikisha zoezi hilo.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.