Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Masasi Mjini Ndg. Prosper Luambano amesema zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa Halmashauri ya Mji Masasi linatarajiwa kuanza siku ya Jumanne, Januari 28, 2025 hadi siku ya Jumatatu, Februari 3, 2025 ambapo kuna jumla ya vituo 127 vya uandikishaji ambavyo vipo katika Vijiji na Mitaa.
Amesema hayo Januari 20, 2025 katika Mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa Jimbo la Masasi Mjini kwa ajili ya kuhamasisha zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo viongozi hao wameelezwa kuhusu mawakala vituoni, idadi ya vituo na masuala mbalimbali kuhusu zoezi hilo.
Amesema Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika zoezi hilo imelenga, kuandikisha wapiga kura wapya ambao wana miaka 18, raia wa Tanzania wataotimiza miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, wanaoboresha taarifa kwa kuhamisha taarifa kutoka jimbo au kata moja kwenda mahali anapoishi, kurekebisha taarifa zilizokosewa wakati wa kujiandikisha, aliyepoteza au kadi kuharibika, zoezi linalengo la kufuata au kuondoa taarifa za watu wasiokuwa na sifa za kupiga kura ikiwemo waliofariki.
Amesema wakati wa uandikishaji kituoni watu wenye ulemavu, wajawazito, wagonjwa, wazee na akina mama wenye Watoto wachanga watakaokwenda nao kituoni hawatapanga foleni.
Viongozi wa Vyama vya Siasa wamesema suala la kuwashirikisha katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ni muhimu zaidi kwao na wanakwenda kufanya uhamasishaji ili kuhakikisha wananchi wote wenye sifa za kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wanashiriki ipasavyo kwa kujiandikisha katika zoezi hilo.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.