Mkuu wa Mkoa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa amekabidhi Tsh milioni 5 kwa shule ya msingi Mkuti iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati akikamilisha ziara yake wilayani Masasi jana 4/4/2019. Akikabidhi fedha hizo mbele ya wanafunzi, watendaji wa Halmshauri ya Mji Masasi pamoja na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Masasi, Mhe.Byakanwa amesema kwamba fedha hiyo itumike kujenga darasa katika shule hiyo. Aidha katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa Mkoa amekabidhi Tsh 525,000 aliyochangisha kutoka kwa watendaji pamoja viongozi mbalimbali wa wilaya waliohudhuria hafla ya makabidhiano hayo.
Pia Mhe. Mkuu wa Mkoa amehaidi kuchangia tofali elfu moja ikiwa ni juhudi za kuunga mkono ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Mkuti inayokabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo. Aidha Mhe. Mkuu wa Mkoa amewaagiza viongozi waliohudhuria hafla hiyo kuhamasisha wananchi hususani wakazi wa eneo la Mkuti ambao watoto wao wanasoma katika shule hiyo kuendelea kuchangia ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwa ni ishara ya kuunga mkono jitihada alizozianzisha Mhe. Rais.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Selemani Mzee, viongozi mbalimbali wa chama na serikali wa Wilaya pamoja na waandishi wa habari na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Mji Masasi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.