Halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara imepitisha Mpango wa Bajeti wa Mwaka 2023/2024 ambapo Halmashauri imekisia kutumia shilingi Milioni 40,375,000 kwa ajili ya ukelezaji wa shughuli za afua za lishe na kugharamia Ununuzi wa Virutubishi lishe ,Maziwa ,na kuhudumia watoto wenye Utapiamlo .
Bajeti hiyo imepitishwa na Afisa Lishe halmashauri ya Mji Masasi Bi Happiness Richard Mlaka katika kikao cha Maandalizi ya Mpango wa bajeti ya lishe kilichofanyika Novemba 19,2022 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji, kikao ambacho kilihudhuriwa na wataalamu wa sekta mbalimbali kutoka Halmashauri ya wilaya ya Masasi ,Halashauri ya Mji Masasi Pamoja na Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Aidha kwa mwaka wa Fedha 2021/2022 Halmashauri ya Mji Masasi ilitumia kiasi cha Shilingi Milioni kumi na Sita Mia Mbili arobaini na Nane elfu (16,248,000) ya Mapato ya ndani sawa na asilimia 100.6 zaidi ya kiasi ambacho kilipangwa ambacho ni Milioni kumi na Sita Mia moja na hamsini na Nne Elfu (16,154,000).
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.