Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imetenga fedha kiasi cha Tsh bilioni 1.628 kwa ajili ya uboreshaji na ukarabati wa hospitali kongwe ya Mkomaindo iliyopo Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ili kuongeza tija ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo Septemba 17, 2023 wakati akitoa salamu za Wizara mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Boma, Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara.
“Wana Masasi wanakushukuru sana Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa hii ya kuongeza tija katika huduma zinazotolewa katika maeneo yetu hapa Masasi”, Mhe. Mchengerwa.
Aidha amesema Serikali imejipanga vyema kwa kuhakikisha mtandao wa barabara katika halmashauri ya Mji Masasi unaongezeka kutoka kilometa 6.9 zilizopo mpaka kilometa 11.2.
“Wanamasasi wanakushukuru sana kwa kazi hiii ya kuongeza mtandao wa barabara na kuongeza taa za barabarani” amesema.
Katika hatua nyingine amesema kwa Mkoa wa Mtwara Serikali imetenga jumla ya Tsh shilingi Bil.6.1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya elimu ili kuongeza mtandao wa elimu sekondari na kwamba kila halmashauri ya mkoa wa Mtwara itakwenda kupata shule moja ya sekondari.
Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara ya Kikazi mkoani Mtwara kwa kuzungumza na wananchi katika uwanja wa boma halmashauri ya Mji Masasi.
Mchengerwa amesema Serikali imetenga fedha kiasi cha Tsh bilioni 1.628 kwa ajili ya uboreshaji na ukarabati wa hospitali kongwe ya Mkomaindo iliyopo Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ili kuongeza tija ya utaoji wa huduma bora kwa wananchi.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo Septemba 17, 2023 wakati akitoa salamu za Wizara mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Boma, Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara.
“Wana Masasi wanakushukuru sana Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa hii ya kuongeza tija katika huduma zinazotolewa katika maeneo yetu hapa Masasi”, Mhe. Mchengerwa.
Aidha amesema Serikali imejipanga vyema kwa kuhakikisha mtandao wa barabara katika halmashauri ya Mji Masasi unaongezeka kutoka kilometa 6.9 zilizopo mpaka kilometa 11.2.
“Wanamasasi wanakushukuru sana kwa kazi hiii ya kuongeza mtandao wa barabara na kuongeza taa za barabarani” amesema.
Katika hatua nyingine amesema kwa Mkoa wa Mtwara Serikali imetenga jumla ya Tsh shilingi Bil.6.1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya elimu ili kuongeza mtandao wa elimu sekondari na kwamba kila halmashauri ya mkoa wa Mtwara itakwenda kupata shule moja ya sekondari.
Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara ya Kikazi mkoani Mtwara kwa kuzungumza na wananchi katika uwanja wa boma halmashauri ya Mji Masasi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.