Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amefungua kituo cha Afya Mbonde kilichopo Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara kikiwakilisha vituo 352 vilivyojengwa kote nchini kwa kipindi cha miezi 18 yaani tangu mwezi Disemba 2017 hadi saa kupitia mpango wa maboresho ya afya.
Mhe. Rais alifanya ufunguzi huo, akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Mtwara na kueleza kuwa kituo cha Afya Mbonde kilichogharimu shilingi milioni 500 ni kati ya vitu 13 vilivyojengwa Mkoani Mtwara vikiwa na uwezo wa kutoa huduma za matibabu mbalimbali ikiwemo upasuaji kwani ina vifaa vya kisasa.
Mhe. Rais ameeleza kuwa “nimekuja kufungua kituo hiki cha Mbonde kwa niaba ya vituo vyote 352 vinavyojengwa nchi nzima baada ya kujiridhisha hatua za ujenzi kwa kila kituo, nawapongeza sana Masasi kwa ujenzi mzuri ulioendana na thamani ya fedha”
Mhe. Rais amefafanua kuwa, Vituo hivi vimejengwa kwa fedha za serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo Benki ya Dunia, Kanada, Serikali ya Ujerumani, UNICEF na wengine, “ nawashukuru sana kwa mchango wao wa kuimarisha afya za wananchi”
Mhe. Rais ameeleza kuwa, Serikali imetumia jumla ya shilingi bilioni 184 kujenga vituo vyote 352 nchi nzima kwa lengo la kuboresha huduma za uhakika za matibabu katikakaribu na maeneo wanayoishi
Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amesema, Serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kujenga vituo vya Afya 352 na Hospitali 67 nchi nzima kwa muda wa miezi 18 ambapo kwa Mkoa wa Mtwara hospitali 3 zinajengwa katika wilaya za Mtwara, Masasi na Nanyamba ukilinganisha na hospitali 77 zilizokuwa zimejengwa tangu Uhuru.
Mhe. Jafo ameeleza kuwa “Ofisi ya Rais TAMISEMI inatekeleza ahadi za Rais kwa kusimamia miradi inayogusa wananchi wanyonge ikiwemo afya kupitia Mpango wa maboresho ya afya kwa katika ngazi za serikali za chini kabisa”
Kwa mujibu wa Mhe. Jafo, Ujenzi wa miradi hii ya afya unatumia mafundi wa kawaida, hivyo kwa miradi yote inayotekelezwa watanzania zaidi 7000 wamepata ajira mbalimbali na kujiongezea kipato.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.