Mkuu wa wilaya ya Masasi Claudia Kitta Septemba 23,2022 amezindua na kukabidhi Miongozo mitatu ya Elimu Kwa Maafisa Elimu kata, Wakurugenzi,maafisa elimu msingi na sekondari,wakuu wa shule,maafisa elimu kata na walimu wakuu,wote wa halmashauri ya Wilaya ya Masasi na Mji.
Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Masasi ambapo Miongozo mitatu ambayo ni Mkakati wa kushiriki kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya Elimu ya Msingi na Sekondari, Changamoto ya uboreshaji Elimu ya Msingi na Sekondari na Uteuzi wa Viongozi katika Sekta ya Elimu.
Katika Uzinduzi huo Bi Claudia amesema kuwa ana Imani na Miungozo iliyozinduliwa na kila wilaya na kata wataisoma Kwa umakini na watayafanyia kazi Yale yaliyoelekezwa Ili kufikia Malengo mahususi katika Elimu Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Masasi Elias Ntiruhungwa amewaomba watumishi wote kuwajibika na kufanya kazi Kwa bidii Ili kuongeza ufaulu Kwa Mkoa wa Mtwara na kuunga Mkono Juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa na Rais Samia suluhu hassani katika kuisimamia Elimu.
Pia amewataka wazazi na walezi kuwa vianara wa kusimamia Malezi ya watoto wao wakiwa nyumbani kuwapa hamasa ya Elimu na kuwahimiza kujisomea
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.