Mkuu wa wilaya ya Masasi Mhe. Lauter John Kanoni amemkabidhi Mkurugenzi wa Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu vibao nane vya kupima urefu/kimo kwa watoto chini ya miaka 5 ambavyo vitasaidia kutambua hali ya udumavu kwa watoto katika vituo vya kutolea huduma za afya Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara.
Mhe. Kanoni alikabidhi vibao hivyo katika kikao cha tathmini ya Lishe Robo ya kwanza 2023/ 2024 kilichofanyika katika Ukumbi wa Jengo la Utawala halmashauri ya Mji Masasi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, Watendaji wa kata 14 za halmashauri ya Mji Masasi, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wawakilishi kutoka Taasisi za dini, Maafisa Lishe na watoa huduma wa vituo vya kutolea huduma za afya Halmashauri ya Mji Masasi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.